Manchester City inayonolewa na kocha mwenye
mafanikio makubwa katika soka barani Ulaya, Pep
Guardiola, wameutumia vyema uwanja wao wa
nyumbani baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1
dhidi ya Sunderland.
City ikicheza mpira wa pasi fupi fupi, ilijipatia bao
la kuongoza mapema tu kwenye dakika ya nne bao
lililofungwa na Sergio Aguero kupitia mkwaju wa
penati.
Raheem Sterling alifanyiwa madhambi ndani ya
eneo la hatari na Patrick van Aanholt.
Baada ya bao hilo City iliendelea kutawala mchezo
huo huku ikishindwa kuwa makini sehemu ya
umaliziaji hivyo kupoteza nafasi nyingi.
Jermain Defoe aliifungia Sunderland bao la
kusawazisha katika dakika ya 71 ya mchezo baada
ya kuwazidi ujanja walinzi wa City.
Hata hivyo City ilipata bao la ushindi dakika tatu
kabla ya mchezo kumalizika, McNair
akiutumbukiza wavuni krosi ya Jesus Navas.
Guardiola leo amemuacha nje kipa namba moja wa
Uingereza, Joe Hart na Yaya Toure ambaye
hakuwemo kabisa kwenye kikosi.
John Stones aliyesajiliwa na Man City siku tatu
zilizopita, amecheza kwa dakika zote tisini,
amekuwa kivutio, akiweza kumudu vyema mfumo
wa Pep.
Licha ya kutawala mchezo huo kwa asilimia 77,
City bado inahitaji marekebisho hasa kwenye
umaliziaji.
Ni dhahiri Guardiola atasajili wachezaji wapya
kabla kufungwa dirisha la usajili Agosti 31.
Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports
Chapisha Maoni