0
Habari kutoka nchini Hispania zinasema
ya kuwa Shirikisho la Soka la Hispania
limemteua Julian Lopetegui kuwa kocha
mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo
akichukua mikoba ya Vicente del
Bosque.

Kocha wa zamani, Del Bosque alijiuzulu
kufuatia kutofurukuta kwenye michuano
ya Ulaya mwaka huu na sasa Lopetegui,
meneja wa zamani wa FC Porto ndiye
atakayeiongoza nchi hiyo kuelekea
katika michuano ya Kombe la Dunia
mwaka 2018.
Ukifuatilia historia yake, Lopetegui
amewahi kuviongoza vikosi cha timu ya
taifa ya Hispania kwa vijana chini ya
umri wa 19, 20 na 21, huku akishinda
taji la michuano ya Ulaya akiwa na
vikosi vya vijana chini ya umri wa miaka
19 na 21. Amewahi kuiongoza Porto
kwa misimu miwili huku akimaliza katika
nafasi ya pili msimu wa 2014-2015 na 3
msimu uliofuata kabla ya kutimuliwa
Januari mwaka huu na nafasi yake
kuchukuliwa na Rui Barros.
Julian Lopetegui
Akiwa na umri wa miaka 49, aliwahi
kucheza katika klabu za Real Madrid na
Barcelona akiwa kipa, kibarua chake cha
kwanza kitakuwa mwezi ujao wakati
watakapochuana na Ubelgiji kwa mchezo
wa kimataifa wa kirafiki.

Chapisha Maoni

 
Top