mema ya jeshi la Polisi. Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa Henry
Mwaibambe,amewataja askari hiyo kuwa ni PC Asuma Mpaji Mwasumbi mwenye namba F.7788,PC Fadhiri Linga mwenye namba G 2122 na PC Veronica Nazaremo Mdeme,wote walikuwa
askari wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Missenyi.
Akifafanua tukio hilo,Mwaibambe amesema askari hao walitenda kosa hulo la fedheha kwa kupiga picha kinyume na maadili ya jeshi hilo mnamo
mwaka 2012 wakiwa kazini,picha ambazo zimesambazwa sehemu mbalimbali za mitandao ya kijamii hapa nchini.
Alisema kuwa PC Fadhiri ndiye aliyehusika na kupiga picha hizo kwa kutumia simu yake ya kiganjani na kuituma katka mitandao mbalimbali
ya kijamii kitendo ambacho ni kinyume cha maadili kwa sababu mbalimbali.
Amezitaja sababu hizo kuwa ni kupiga picha wakati wakijua kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha maadili ya jeshi hilo pamoja na kuituma picha
hiyo kwenye mitandao mbalimbali.
Aidha,Mwaibambe amekiri kuwa picha husika inayoonekana kwenye mitandao ni picha halisi ambayo haijachakachuliwa,hivyo ni wazi kila
askari kujua kuwa maadili ya kijeshi yapo kisheria na askari yeyote anafundishwa namna ya kuishi
katika maisha ya utumishi wa jeshi la Polisi.
Chapisha Maoni