Msanii maarufu wa maigizo Amr Athuman ‘King Majuto’ amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jengo la Mwaisela wodi namba mbili katika chumba cha uangalizi maalumu ICU
Taarifa iliyotolewa na afisa habari wa Chama cha Waigizaji Kinondoni, Masoud Kaftany imeeleza kuwa Mzee Majuto amelazwa hospitalini hapo na tayari madaktari wameanza kufanya vipimo ili kubaini ugonjwa unaomsumbua.
Mzee Majuto amelazwa huku ikiwa umepita mwezi mmoja baada ya kutoka katika matibabu nchini India alikokwenda kufanyiwa matibabu ya nyonga na upasuaji wa tezi dume.
Chapisha Maoni