0
 Mvua kali sana inayonyesha sasa katika mji wa Kartepe nchini Uturuki, imesababisha tena mchezo kati ya Simba na Ittihad Riadi de Tanger mchezo wa kirafiki usichezwe.

Kutokana na hali hiyo ya mvua kali, kocha wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems amewaambia wachezaji wake wapumzike hadi hali itakapokuwa nzuri.

"Hali imekuwa mbaya mvua inanyesha sana, hivyo mechi haipo mpaka itakapopangwa," alisema meneja wa Simba, Richard.
Huo ulikiwa mchezo wa pili baada ya ule wa awali na Moloudia Oujda FC ambao pia ilivunjima kwa sababu ya mvua katika dakika ya 65 na matokeo yalikuwa sare bao 1-1.

Chapisha Maoni

 
Top