Marekani baada ya kuwahudumia wagonjwa wa Ebola Afrika Magharibi.
Mwongozo huo unapendekeza kuwa
wanaoshukiwa kuwa katika hatari ya
kuwaambukiza wengine watazuiliwa nyumbani kwao; ingawa majimbo tofauti yatakuwa na uhuru wa kutoa mwongozo thabiti zaidi.
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa amepinga hatua hizo za kuwaweka karantini walioathirika.
Mlipuko wa ugonjwa wa ebola afrika magharibi umewaathiri zaidi ya watu 10,000 na kuwaua takriban watu 5,000.
Tangazo hilo la Marekani linajiri baada ya muuguzi aliyelalama kuhusu kutengwa kwake katika jimbo la
New Jersy kutakiwa kurudi nyumbani.
Christie wa New Jerzy Akikaidi mahitaji hayo mapya ,gavana wa New
Jerzy Chris Christie alitetea mahitaji hayo ya karantini aliyowekewa Kaci Hickox wakati alipowasili kutoka Sierra Leone .
Ameongezea kuwa wataendelea kuchukua hatua kama hizo.
Msimamo huo unatofautiana na ule wa katibu mkuu umoja wa mataifa Ban Ki Moon ambaye awali alisema kuwa wale wanaotaka kutoa msaada
wasiwekewe vikwazo ambavyo haviambatani na
sayansi.
Alisema kwamba wale wamepata maambukizi wanafaa kusaidiwa na sio kutengwa. Watu walioathirika hawawezi kuambukiza hadi watakapoanza kuonyesha dalili za ugonjwa huo.
Chapisha Maoni