0
Naibu waziri mkuu wa zamani aliyeshtakiwa kwa kufanya mapenzi na mshirika wake mmoja wa kisiasa alihukumiwa miaka mitano gerezani.
Bwana Anwar anadai kuwa mashtaka hayo yalichochewa na maadui wake wa kisiasa. Mamia ya wafuasi wake wamesongamana mahakamani kuandamana dhidi ya hukumu iliyotolewa dhidi yake.

Wafuasi wake wanaendelea kuuza tisheti zilizoandikwa kuwa wanaitisha haki ya Bwana Anwar.
Nje ya mahakama utadhani ni mkutano wa hadhara wala sio kesi inayohusiana na uhalifu wa mapenzi. Ushoga ni haramu katika taifa hili lenye Waislamu
wengi lakini ni vigumu sana kupata watu
wameshtakiwa.
Mawakili wa Bwana Anwar wanatarajiwa
kuwasilisha mahakamani kuwa uchunguzi wa DNA uliotumiwa ulivurugwa katika juhudi za maadui
wake wa kisiasa kumharibia sifa.
Maafisa wa Serikali wamekanusha kuhusika katika kesi hiyo na wanasema kuwa kesi ya Bwana Anwar
imeshughulikiwa na Mahakama huru.
Mwanasiasa huyo mkongwe ameshtakiwa kuwa alifanya tendo la ngono na mshirika wake wa
kisiasa mwanamume.

Hili ni shtaka la pili la ushoga linalomkabili Bwana Anwar tangu atimuliwe Serikalini mwaka 1998.

Chapisha Maoni

 
Top