zinasema kuwa waendesha mashtaka wa
Afrika Kusini watakata rufaa nyingine
tena ili kupinga hukumu wanayoielezea
kuwa ni ndogo mno aliyopewa Oscar
Pistorius ya miaka 6 pekee jela kwa
kosa la kumuua mpenzi wake mwaka
2013.
Mchezaji bingwa huyo wa zamani wa
mbio za Olimpiki za walemavu mwenye
umri wa miaka 29, alihukumiwa miaka 6
jela na jaji Thokozile Masipa baada ya
kupatikana na kosa hilo la kuumua
Reeva Steenkamp siku ya wapendanao
mwaka 2013.
Kwenye rufaa ya awali, alikuwa
amekabiliwa na uwezekano wa kufungwa
jela zaidi ya miaka 15. Uamuzi huo
ulikuwa umetolewa baada ya
kubatilishwa kwa hukumu ya awali ya
kuua bila kukusudia wakati jaji huyo
huyo Thokozile Masipa alimpa kifungo
cha miaka mitano tu jela akisema
Pistorius hakukusudia kuua na alidhania
amevamiwa na mwizi ndipo akafyatua
risasi bila kujua ni Reeva Steenkamp
aliyekuwa nyuma ya mlango wa bafu.
Kwa kutoa hoja hiyo inayopingwa vikali
na kambi ya mwendesha mashtaka
wakisema Pistorius alijua bayana
aliyekuwa akimfyatulia risasi ni Reeva
kwani walikuwa wote nyumbani kwake
siku hiyo ya Valentine, na huenda
wapenzi hao walikuwa na ugomvi baina
yao. Upande wa utetezi ulikuwa
umesema hawangekata rufaa kwa
hukumu hiyo ya pili ya miaka 6. Upande
wa mwendesha mashtaka unasema
iwapo hawatapigania haki, kwamba
Pistorius apewe kifungo kirefu
inavyostahili kwa makosa hayo ya
mauaji, basi itakuwa mfano mbaya
utakaofanya mfumo wa sheria Afrika
Kusini udharauliwe!
Kwa upande mwingine, wazazi wa Reeva
wamesema wanaunga mkono juhudi
zote zinazofanywa na waendesha
mashtaka kupata haki, na kwamba kifo
cha mtoto wao kimewaathiri vibaya sana
kiasi cha kuwasababishia maradhi!
Wanapanga kufungua wakfu kwa jina la
mtoto wao Reeva aliyekuwa anajulikana
sana kama mwanamitindo mwenye sura
ya kuvutia sana
Chapisha Maoni