0

MSHAMBULIAJI wa kimataifa
wa Tanzania, Mbwana Ally
Samatta ‘Sama Goal’
amefunga penalti ya tatu
timu yake, KRC Genk ya
Ubelgiji ikishinda kwa
penalti 4-2 dhidi ya wenyeji
Buducnost usiku Uwanja
wa Pod Goricom mjini
Podgorica, Montenegro katika
mchezo wa marudiano
Raundi ya Pili ya mchujo wa
kufuzu hatua ya makundi ya
Europ League.
Timu hizo zilifikia kwenye
matuta baada ya sare ya
jumla ya 2-2, Genk ikianza
kushinda 2-0, mabao ya
Neeskens Kebano kwa
penalti dakika ya 16 na
Samatta dakika ya 79
Alhamisi iliyopita na usiku
huu Buducnost wamelipa
kisasi kwa ushindi wa 2-0,
mabao ya Radomir Dalovic
dakika ya
kwanza na Milos Raickovic
dakika ya 39.
Katika mikwaju ya penalti,
mbali na Samatta wengine
waliofunga upande wa Genk
ni Thomas Buffel, Bryan
Heynen na  Dries Wouters ya
mwisho, wakati za
Buducnost zilifungwa
na Risto Radunovic
na Radomir Dalovic,
huku Momcilo Raspopovic
na Luka Mirkovic wakikosa.
Genk ilimaliza mchezo huo
pungufu baada ya kungo
wake Mghana, Bennard Yao
Kumordzi kutolewa kwa kadi
nyekundu dakika ya 75.
Sasa Genk itamenyana na
mshindi wa mechi kati ya BK
Hacken ya Sweden na Cork
City FC ya Ireland katika
Raundi ya Tatu, mechi ya
kwanza ikichezwa Julai 28
nyumbani na marudiano
Agosti 4 ugenini.
Mchezo wa kwanza baina ya
BK Hacken na Cork City FC
ulimalizika kwa satre ya 1-1
nchini Sweden. Ikumbukwe
timu zitakazoshinda
zitakwenda hatua ya mwisho
ya mchujo kuwania
kupangwa kwenye makundi,
ambako sasa vigogo kama
Manchester United ya
England wataanzia huko.

Kikosi cha FK Buducnost
Podgorica kilikuwa:
Dragojevic, Radunovic,
Vukcevic, Vusurovic,
Mitrovic, Vujovic/Hocko dk62
Raickovic, Raspopovic,
Mirkovic, Janketic/Pejakovic
dk52 na Dalovic.

KRC Genk: Bizot, Castagne,
Dewaest, Kumordzi, Uronen,
Ndidi, Buyens/Heynen dk45,
Buffalo, Bailey, Karelis/
Wouters dk74 na Samatta.






Chz
Ben Zubery
Posted Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top