0

Mkude alikuwa nchini Afrika Kusini kwenye
majaribio ya kucheza soka la kulipwa kwenye
klabu ya Bidvest Wits na amepewa mtihani mzito
na Omog ili kurejea katika namba yake
Kocha wa Simba Joseph Omog, amemkaribisha
kambini Kiungo wake Jonas Mkude na kutaka
afanye kazi ya ziada ili kurejea nafasi yake.
Omog ameiambia Goal kuwa Mkude ni mchezaji
mzuri lakini hajamuona siku nyingi ukilinganisha
na wachezaji akianza nao mazoezi Kambini
Morogoro.
"Namfahamu ni mchezaji mzuri ana uwezo
mkubwa wa kukaba na hata kufunga akiwa mbali
lakini anatakiwa kunionyesha mazoezi kabla
sijapangua kikosi,"amesema Omg
Mcameroon huyo amesema anayaka kuwa na
kikosi cha wachapakazi ambao watatekeleza kwa
asilimia 85 kazi atakayowatuma uwanjani ya
kusaka pointi tatu katika kila mchezo.
Mkude alikuwa nchini Afrika Kusini kwenye
majaribio ya kucheza soka la kulipwa kwenye
klabu ya Bidvest Wits na amerejea juzi baada ya
kumaliza wiki mbili za majaribio hayo na majibu
yanatarajiwa kutumwa siku yoyote kuanza kesho
Jumatatu.



Posted Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top