Ripoti kutoka mji mkuu wa Sudan Kusini Juba ,zinasema kuwa mili mingi imepelekwa katika hospitali kuu ya mji huo baada ya ufyatulianaji
mkali wa risasi kuibuka karibu na nyumba ya rais siku ya Ijumaa.
Idadi ya watu waliouawa hatahivyo haijulikani.
Ufyatulianaji huo ulianza wakati ambapo rais Salva Kiir na makamu wake Riek Machar walikuwa
wakijadiliana kuhusu ghasia siku ya Alhamisi baada ya wanajeshi watano wa serikali kuuawa
katika vita vya pande pinzani.
Viongozi wote wawili wametaka kuwepo kwa utulivu.
Ghasia hizo ni mbaya zaidi kuwahi kutokea tangu makamu wa rais Riek Machar kurudi mjini Juba
mnamo mwezi Aprili na vilevile zinajri wakati ambapo taifa hilo changa zaidi duniani liko katika
harakati za kuadhimisha mwaka wa tano tangu lijipatie uhuru wake.
BBC
Chapisha Maoni