Mshambulizi wa Ufaransa na Juventus Paul Pogba
ameomba kuihama klabu hiyo ya Italia.
Magazeti ya michezo nchini Italia yamechapisha
habari hiyo kama kichwa kuwa Mfaransa huyo
mwenye umri wa miaka 23 ameomba aruhusiwe
kuondoka kwani posho lake linavutia.
La Gazzetta dello Sport liliongoza na kichwa
''Pogba ameamua kuondoka Juventus''
Gazeti hilo linadai kuwa mfaransa huyo amekwisha
kubaliana posho lake na Mashetani wekundu huku
ikisisitiza kuwa sababu kuu iliyomfanya makamu
wa mwenyekiti wa klabu hiyo bwana Ed Woodward
asiandamane na timu ya Manchester united
kwenda Uchina ilikuwa ni kwa sababu alikuwa
ameamua kuandaa ombi rasmi la kumsajili
mchezaji huyo wao wa zamani.
I Corriere dello Sport nalo linadai kuwa Pogba
“anarejea Manchester United kwa kitita cha Euro
milioni €125 million,”
Jarida lingine la michezo lenye makao yake huko
Turin, Tuttosport nalo linasema kuwa Pogba
ameomba ruhusa ya kuondoka.
Tuttosport, linasema kuwa ''Pogba atatia sahihi
mkataba wa kipekee na wenye thamani ya pesa
nyingi kupindukia utakaodumu kwa miaka mitano''
Wakala wake Mino Raiola amenukuliwa na jarida
lingine akikanusha kuwa ameanza mazungumzo
na klabu ya manchester United dukuduku zinadai
kuwa ombi la kimsingi la Manchester United la
Euro milioni moja (£85m) limekataliwa.
Aidha inadaiwa kuwa Woodward na Raiola
wamekutana na meneja wa Juventus Beppe
Marotta na kuomba kandarasi yake kwa Euro
€101m lakini ombi lao likakataliwa.
Iwapo mkataba huu utafaulu, mfaransa huyo ndiye
atakayekuwa mchezaji aliyegharimu kitita kikubwa
zaidi cha fedha katika historia ya kandanda.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni