Mkufunzi mpya wa Manchester City,Pep Guardiola,
amesajili ushindi wake wa kwanza tangu atue
Manchester City baada ya kuwaongoza mabingwa
hao wa zamani wa ligi kuu ya Uingereza kuwalaza
Borussia Dortmund katika kinyang'anyiro cha
kutafuta mabingwa wa vilabu vya kimataifa huko
China.
Kipa chipukizi wa Man City Angus Gunn, 20,
aliokoa mkwaju wa penalti wa Mikel Morino na
kuwahakikishia vijana wa Pep ushindi wa mabao
6-5.
Mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa
Longgang ulioko Shenzhen ilikuwa imeishia sare
ya 1-1 katika muda wa kawaida.
Sergio Aguero alikuwa ameiweka Man City kifua
mbele mapema katika mechi hiyo lakini
mshambulizi chipukizi wa Dortmund Christian
Pulisic, mwenye umri wa miaka 17,
kuwasawazishia wajerumani hao katika muda wa
majeruhi.
Hii ndio ilikuwa mechi ya kwanza kwa Man City
baada ya mechi iliyokuwa imepangwa awali dhidi
ya vibonde wao wa jadi kutoka Uingereza
Manchester United kuahirishwa kufuatia mvua
kubwa iliyonyesha mjini Beijing.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni