Thienry Henry, amesema bado anaipenda Arsenal,
na kuondoka kwake kwenye benchi la ufundi la
kikosi cha vijana siyo mwisho wa kuisaidia timu
hiyo.
Mshambuliaji huyo wa zamani Arsenal amesema
hana kinyongo na klabu hiyo baada ya kuacha
kukifundisha kikosi cha vijana cha timu hiyo hivi
karibuni.
Henry mfungaji wa muda wote wa klabu ya
Arsenal, aliacha kukinoa kikosi cha U-18, baada ya
kuambiwa na Arsene Wenger achague kazi moja
kati ya hiyo, au aendelee na uchambuzi wa soka
kwenye kituo cha Skysports.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya
Ufaransa, alisema kuwa bado anaipenda Arsenal na
alichokuwa anakifanya kwenye kikosi cha vijana
cha timu hiyo, ni kutafuta uzoefu wa kufundisha
wakati huu akisubiri kupata leseni ya daraja A ya
ukocha barani Ulaya.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni