0

Straika wa Azam FC, Kipre Tchetche raia wa Ivory Coast.



HUKU straika wa Azam FC, Kipre Tchetche raia wa
Ivory Coast akigoma kurejea nchini kujiunga na
wenzake, imebainika kuwa mpango wake wa
kutua Yanga upo na atakuwa mchezaji ghali
kuliko wote klabuni hapo. Katika kikosi cha Yanga hivi sasa, Mzambia,
Obrey Chirwa ndiye ghali zaidi baada ya usajili
wake kugharimu zaidi ya Sh milioni 200. Hivi karibuni uongozi wa Azam ulitangaza kama
kuna timu inamuhitaji straika wao huyo, iende
mezani kwao kuzungumza na wakikubaliana basi
watamuachia kwa moyo mmoja.
Azam ilisema thamani ya Muivory Coast huyo ni
dola 150,000 ambazo ni zaidi ya Sh milioni 300.
Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema kuwa
kwa sasa hivi mipango inafanywa kuhakikisha
Tchetche anakuwa mchezaji wao, lakini
watamaliza kila kitu katika usajili wa dirisha dogo
hapo baadaye. Championi lilipozipata taarifa hizo, likamtafuta
Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit, ambaye
kwanza alishtuka kusikia taarifa hizo na kudai
kuwa ndiyo kwanza anazisikia lakini akabainisha
kwa sasa hawana mpango naye labda hapo
baadaye. “Hizo taarifa bado sijazipata, lakini ukiangalia hivi
sasa kikosi chetu kina wachezaji saba wa kigeni
ambao ndiyo wanaotakiwa kwa mujibu wa TFF
(Shirikisho la Soka Tanzania), hivyo hakuna nafasi
yake labda hapo baadaye,” alisema Deusdedit.
Wachezaji wa kigeni wa Yanga ni Chirwa raia wa
Zambia, Amissi Tambwe (Burundi), Vincent
Bossou (Togo), Thabani Kamusoko na Donald
Ngoma (wote Zimbabwe), Haruna Niyonzima na
Mbuyu Twite (wote Rwanda).



Posted Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top