zamani wa AC Milan, Chelsea na Real
Madrid. “Anahitaji likizo ndefu kidogo
kwa sababu amecheza mechi nyingi,
lakini atakaporejea atakuwa muhimu
kwenye kikosi chetu,” ameongeza kocha
huyo. Imedaiwa ya kuwa mchezaji
Thomas Muller anahitaji mapumziko ya
muda mrefu, haya ameyasema kocha
mpya wa klabu ya Bayern Munich, Carlo
Ancelotti. Kocha huyu amesema kwamba
ameyatazama kwa makini mashindano
ya Kombe la Mataifa ya Ulaya na
kugundua kwamba Muller amechoka na
hivyo yeye kama kocha wa Bayern
anashauri mchezaji huyo apumzishwe
katika msimu ujao wa Bundesliga.
Mchezaji Muller ambaye katika kikosi
cha Bayern amekuwa alama ya ushindi
kwa miaka minne sasa, hakuwa kwenye
wakati mzuri wakati wa Euro 2016 na
ameshindwa kuisaidia Ujerumani kuvuka
kwenye hatua ya nusu fainali. Ancelotti
akiongea kwenye mkutano wa waandishi
wa habari amesema kwamba
ameshauriana na Muller jinsi ya
kumrejesha kwenye makali yake na
kugundua kwamba yanahitajika maamuzi
ya hekima zaidi.
Chapisha Maoni