ya kocha na nyota wa zamani wa Real
Madrid, Zinedine Zidane, stori zilikuwa
kubwa mitandaoni, Zidane anaripotiwa
na mtandao wa dailyamail.co.uk kuwa
ametofautiana na rais wa klabu ya Real
Madrid, Fiorentino Perez.
Rais Perez na Zidane wanasemekana
kupishana kutokana na Zidane kutokuwa
tayari kumjumuisha kinda Martin
Odegaard kikosini mwake kinachoanza
maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu,
Zidane ametaja kutaka kumuacha Martin
Odegaard mwenye umri wa miaka 17
kutokana na maendeleo yake kikosini
kuwa tofauti na matarajio.
Na zaidi, sababu nyingine iliyomfanya
Zidane amuache mchezaji huyo kwenye
kikosi chake ni kutokana na kutokuwa na
mipango naye katika msimu huu, hivyo
alikuwa anataka arudi katika kikosi cha
wachezaji wa akiba Castilla!
Chapisha Maoni