Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu Tanzania
‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa,
ametangaza wachezaji 20 watakaounda kikosi
kitakachosafiri mwishoni mwa mwezi huu kwenda
Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa
kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya
Afrika (AFCON 2017) dhidi ya timu ya taifa ya nchi
hiyo, Super Eagles.
Licha ya mchezo huo wa Septemba 3, 2016 kuwa
sehemu ya mchuano wa kuwania nafasi ya
kucheza fainali hizo za AFCON 2017 huko Gabon,
lakini utakuwa ni wa kukamilisha ratiba baada ya
Misri kufuzu kutoka kundi G ambalo mbali ya
Nigeria na Tanzania, pia ilikuwako Chad ambayo
iliyojitoa katikati ya mashindano.
“Tanzania hatuwezi kupuumza mchezo huu,
tumeuchukulia serious (kwa umakini) kabisa kwa
sababu tunacheza ugenini ambako matokeo
mazuri yanaweza kutusongesha mbele na kuingia
ndani ya timu 99 bora katika viwango vya FIFA,”
amesema Mkwasa.
Katika kikosi chake, Mkwasa ametangaza
kutomjumuisha Mshambuliaji wa Kimataifa,
Thomas Ulimwengu anayecheza klabu ya TP
Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
(DRC) kutokana na majeruhi ya paja kama ilivyo
kwa Juma Abdul wa Young Africans ambaye
aliumia katika mchezo wa kuwania Kombe la
Shirikisho dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria.
“Timu itaingia kambini Agosti 28, itakaa kambini
kwa siku tano kabla ya kusafiri kucheza mchezo
huo wa kukamilisha ratiba ambao Misri tayari
wameshafuzu fainali za Afrika,” amesema Mkwasa
na kuongeza kuwa kuna mchezaji wa Tanzania,
Said Carte Mhando anamfuatilia ili ikiwezekana
baadaye amwite kuchezea timu ya taifa. Anakipiga
Klabu ya Brencia Calcio ya Italia.
Wachezaji walioitwa:
Makipa-
Deogratius Munishi – Young Africans
Aishi Manula – Azam FC
Mabeki
Kelvin Yondani - Young Africans
Vicent Andrew - Young Africans
Mwinyi Haji - Young Africans
Mohamed Hussein – Simba SC
Shomari Kapombe - Azam FC
David Mwantika - Azam FC
Viungo
Himid Mao - Azam FC
Shiza Kichuya – Simba SC
Ibrahim Jeba – Mtibwa Sugar
Jonas Mkude – Simba SC
Muzamiru Yassin – Simba SC
Juma Mahadhi - Young Africans
Farid Mussa Tenerif ya Hispania
Washambuliaji
Simon Msuva - Young Africans
Jamal Mnyate – Simba SC
Ibrahim Ajib – Simba SC
John Bocco - Azam FC
Mbwana Samatta - CK Genk ya Ubelgiji
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni