ni kocha wa El Masry,
Hossam Hassan anaamini
anaweza kuwazima wenyeji
Kampala City Council
Authority (KCCA) katika
mchezo wa kwanza wa
mchujo wa kuwania hatua ya
makundi ya Kombe la
Shirikisho Afrika leo mjini
Kampala.
Hossam ameiambia Bin
Zubeiry Sports - Online jana
mjini Kampala kwamba licha
ya kuwa taarifa chache za
wapinzani wao, wapo hapaa
kwa ajili ya kushinda
kuelekea mchezo wa
marudiano.
“Tumekuja kufuata matokeo
mazuri Kampala ambayo
itafanya mchezo wetu wa
marudiano uwe mwepesi,”
amesema Hossam, ambaye
ni kati ya ndugu wawili
maarufu waliovuma kwenye
soka ya Misri, kaka yake,
Ibrahim ni Mkurugenzi wa
Ufundi wa timu hiyo.
Kocha wa El Masry, Hossam
Hassan (kushoto) akiwa na
Mkurugenzi wake wa Ufundi
na kaka yake, Ibrahim
Hassan
Mkongwe huyo wa umri wa
miaka 50, si mgeni wa soka
ya Afrika akiwa ameshinda
mataji kibao na vigogo wa
Misri, Al Ahly na Zamalek na
amesema KCCA ni timu
madhubuti Uganda, lakini
timu yake itacheza kiufundi
kupata matokeo mazuri
wanayotaka.
Wachezaji wawili tegemeo,
Ahmed Shoukry na Ahmed
Gomaa aliyefunga katika
ushindi wa 2-0 wa Masry
dhidi ya ENPPI kwenye Ligi
Kuu ya Misri Jumapili
iliyopita, pia wamesafiri na
timu hiyo.
Wakati Masry ni ya tatu
kwenye Ligi Kuu ya Misri,
wenyeji wao, KCCA walipanda
hadi nafasi ya pili kwenye
Ligi ya Ugandan Jumanne
iliyopita baada ya ushindi wa
2-1 dhidi ya Bright Stars.
Mabingwa wa Uganda
walitolewa na mabingwa wa
Afrika, Mamelodi Sundowns
ya Afrika Kusini kwa jumla ya
mabao 3-2 kwenye hatua ya
32 Bora ya Ligi ya Mabingwa
Afrika.
Kocha wa KCCA, Mike Mutebi,
amesema hawawezi
kuwatukuza wapinzani wao
kutoka Misri. “Tunafahamu
aina ya soka yao, ambayo ni
kupiga pasi ndefu, lakini
tunajua pa
kuwakamatia,”alisema.
Pamoja na hayo, Waganda
hao watamkosa beki
tegemeo, Joseph Ochaya,
aliyejiunga na Lusaka
Dynamos yab Zambia wiki
mbili zilizopita.
RATIBA MECHU ZAMCHUKO
WA KUWANIA HATUA YA
MAKUNDI KOMBE LA
SHIRIKISHO
Leo, Jumamosi Aprili 8,
2017
CF Mounana (Gabon) vs
ASEC Mimosas (Ivory Coast)
Bidvest (Afrika Kusini) vs
Smouha (Misri)
CNaPS (Madagascar) vs
Recreativo do Libolo (Angola)
KCCA (Uganda) vs El Masry
(Misri)
Yanga SC (Tanzania) vs MC
Alger (Algeria)
Jumapili Aprili 9, 2017
FUS Rabat (Morocco) vs MAS
Fes (Morocco)
Rangers (Nigeria) vs Zesco
(Zambia)
RC Kadiogo (Burkina Faso)
vs CS Sfaxien (Tunisia)
Ports Authority (Gambia) vs
Hilal Obeid (Sudan)
Port Louis (Mauritius) vs
Club Africain (Tunisia)
Barrack Young Controllers
(Liberia) vs Supersport
(Afrika Kusini)
AS Tanda (Ivory Coast) vs
Platinum Stars (Afrika Kusini)
Horoya (Guinea) vs Ittihad
Tangier (Morocco)
AC Leopards (Kongo) vs
Mbabane Swallows
(Swaziland)
TP Mazembe (DRC) vs JS
Kabylie (Algeria)
Jumamosi Aprili 15, 2017
Rivers United (Nigeria) vs
Rayon Sports (Rwanda)
Chapisha Maoni