Klabu ya Crystal Palace imevunja rekodi yake ya
usajili baada ya leo mchana kumsajili
mshambuliaji,Mbelgiji Christian Benteke,kutoka
klabu ya Liverpool kwa ada ya £27m.
Benteke,25,amesaini mkataba wamiakka minne
wa kuitumikia Crystal Palace baada ya kufuzu
vipimo vya afya.
Benteke alijiunga na Liverpool msimu uliopita
akitokea Aston Villa kwa ada ya £32.5m lakini
kutokana na kuwa majeruhi wa mara kwa mara
alijikuta akiwa mshambuliaji chaguo la tatu
nyuma ya Divock Origi na Roberto Firmino.
Benteke ameihama Liverpool baada ya kuifungia
mabao 10 katika michezo 42.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni