Ligi ya mabingwa Ulaya hatua ya nusu fainali mechi za mkondo wa pili zinaendelea leo kwa mechi moja pekee kupigwa ikiwa ni mechi ya marudiano baina ya wenyeji Juventus dhidi ya
Monaco ya Ufaransa.
Monaco itasafiri kuwavaa Juventus ikiwa na kikosi kilichosheheni vijana wengi ambao wameifanya timu hiyo kuwa moja kati ya timu zilizofunga
magoli mengi sana katika ligi za Ulaya ikiwa na leo moja tu la kuweza kupindua matokeo ya bao 2-0 ambayo Juventus waliyapata wiki iliyopita jijini Monaco.
Kijana mwenye miaka 18 Kylian Mbappe Lotin ni mmoja wa washambuliaji wanaotisha katika kuzifumania nyavu pinzani akicheza pamoja na
mkongwe Radamel falcao kwenye safu ya ushambuliaji ya Monaco.
Monaco hawatakua na kazi rahisi kuifunga Juventus ambayo inasifika kwa kuwa na safu bora ya ulinzi ikiongozwa na kipa mkongwe Gianluigi
Buffon ambaye ni nahodha na mchezaji mkongwe zaidi katika kikosi hicho.
Monaco watatakiwa kushinda bao 3-0 ili kuweza kuvuka hatu hii na kutinga fainali ya ligi ya mabingwa ulaya kwa mara ya kwanza baada ya miaka kadhaa.
mechi hii ya leo inatarajiwa kuanza saa 4 kasoro kwa saa za hapa Nyumbani Tanzania
Chapisha Maoni