0

Mzee Ibrahim Omary Akilimali anatajwa kuwa
mmoja ya wale wanaodaiwa kumfanyia
'chokochoko'Mwenyekiti wa klabu ya Yanga
Yusuph Manji hadi kupelekea kutangaza kujiuzulu
wadhifa wake jana.
Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana mapema leo,
Mzee Akilimali aliitwa kwenye kikoa cha uongozi
wa klabu hiyo ambayo inafanya juhudi za
kumshawishi Manji asijiuzulu.
Mzee Akilimali amewaomba radhi wapenzi na
washabiki wa klabu ya Yanga kutokana na kauli
zake alizozitoa kwenye vyombo vya habari.
Lakini amesisitiza kuwa nia yake ni kuitaka Yanga
iwe moja na Manji aonyeshe heshima kwa wazee
wa klabu hiyo.
“Manji ni kijana wetu, sisi wazee nikiwemo mimi
tulichangia yeye kuingia ndani ya Yanga, hata
mimi ndiye niliyemkabidhi ngao ya uchifu wa
Yanga, sasa hapo katikati alikuwa hatushirikishi
sisi wazee kama ilivyokuwa zamani.
“Akawa anafanya maamuzi anayoyajua yeye, nia
yetu sisi wazee ni kuifanya Yanga iwe moja kuwe
na mshikamano, unajua Manji ametutoa mbali, sisi
ni Yanga moja, kwa mapenzi yangu yote nataka
Yanga iwe kitu kimoja. Yanga ni moja na hakuna
mpasuko.
Hata hivyo licha ya kuomba radhi, katika kikao cha
dharura kilichofanywa na Umoja wa matawi ya
klabu ya Yanga, kimeazimia kwa kauli moja
kumsimamisha uanachama mzee Ibrahim Akilimali
kwa muda usiojulikana.
Wengine walitaka afutiwe kabisa uanachama wake.
Pia wametaka kuvunjwa mara moja kwa Baraza la
Wazee kwa kuwa halitambuliki kwenye Katiba ya
Klabu ya Yanga.
Wamewataka wazee wasajiliwe kwenye matawi ya
wanachama.
Pia wameamua kuwa ni haramu kwa mwanachama
yeyote wa klabu ya Yanga kuzungumza masuala
ya klabu hiyo kwenye vyombo vya habari bila
kupata ruhusa ya klabu.
Kuhusu Manji, Mwenyekiti wa klabu hiyo aliyetishia
kujiuzulu, atatoa taarifa rasmi kwa vyombo vya
habari juu ya hatma yake.
Ila kuna taarifa kwamba ameamua kusitisha azma
yake ya kujiuzulu.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top