0

MENEJA wa West Ham United Slaven Bilic
amesema Straika wa Chelsea Diego Costa
alistahili Kadi Nyekundu kwenye Mechi ambayo
West Ham walichapwa 2-1 na Chelsea Jana Usiku
huko Stamford Bridge.
Costa ndie aliefunga Bao la Pili na la ushindi kwa
Chelsea katika Dakika ys 89.
Lakini, kabla ya hapo, akiwa tayari ashatwangwa
Kadi ya Njano, Costa alimchezea Rafu Kipa wa
West Ham Adrian lakini Refa Anthony Taylor alitoa
Frikiki bila ya kumpa Kadi ya Njano ambayo
ingemfanya astahili Kadi Nyekundu na kutolewa
nje.
Kubaki kwa Costa Uwanjani kulimfanya ampe
Meneja wao mpya Antonio Conte ushindi wao wa
kwanza katika Mechi yao ya kwanza ya Msimu
mpya wa Ligi Kuu England.
Akiongea na Sky Sports, Bilic alisema: "Tayari
alikuwa na Kadi na alicheza rafu na sidhani ni
kusudi lakini alichelewa na alipaswa kupewa Kadi
nyingine!"


Kwenye Mechi hiyo, West Ham walipata pigo
baada kulazimika kumtoa nje Mchezaji wao mpya
kutokana Ghana, Andre Ayew, alieumia Pajani
katika Dakika ya 35.

LIGI KUU ENGLAND
Msimu Mpya 2016/17
Ijumaa Agosti 19
22:00 Man United v Southampton

Jumamosi Agosti 20
14:30 Stoke City v Man City
17:00 Burnley v Liverpool
17:00 Swansea v Hull
17:00 Tottenham v Crystal Palace
17:00 Watford v Chelsea
17:00 West Brom v Everton
19:30 Leicester City v Arsenal

Jumapili Agosti 21
15:30 Sunderland v Middlesbrough
18:00 West Ham v Bournemouth



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top