0

Mwanariadha Mjamaica Usain Bolt ameendelea
kuwa tishio katika vita ya mbio fupi katika
michuano ya Olympic.
Bolt,29,usiku wa kuamkia leo amefanikiwa
kushinda medali ya dhahabu ya michuano hiyo
baada ya kushinda mbio za mita 100 akitumia
sekunde 9.81.
Mjamaica huyo amembwaga mpinzani wake
Mmarekani Justin Gatlin ambaye amechukua
medali ya fedha akitumia sekunde 9.89 huku
medali ya shaba ikienda kwa Mcanada Andre de
Grasse aliyetumia sekunde 9.91
Bolt amekuwa mwanariadha pekee kuwahi
kushinda medali 3 za dhahabu za mita 100 katika
michuano mitatu ya Olympic.
Hata hivyo Bolt hajaifikia rekodi yake ya dunia
katika Olympic ya mbio za mita 100 aliyoiweka
London 2012 ambapo alitumia sekunde 9.63.
Usain Bolt katika michuano hii ana ndoto za
kuweka rekodi ya kupata medali tatu ili
kukamilisha Triple-Triple katika Olympic, mwaka
2008 na 2012 katika Olympic alipata medali za
dhahabu katika mbio za mita 100,200 na 4✖️100
Relay, hivyo anataka kufanya hivyo na sasa.
Mpaka sasa katika michuano ya Olympic Bolt ana
jumla ya medali 7 za dhahabu.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top