Antonio Conte Meneja wa Chelsea ameanza vyema
kibarua chake kwenye ligi kuu ya Uingereza baada
ya timu yake kuilaza West Ham mabao 2-1 katika
mchezo uliopigwa katika dimba la Stamford
Bridge.
Chelsea ilistahili kupata ushindi katika mchezo huo
kutokana na kiwango walichoonyesha tangu dakika
ya kwanza.
Mabao yote ya mchezo huo yalipatikana kipindi
cha pili, Eden Hazard akianza kuifungia Chelsea
kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 47 baada
ya Oscar kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la
hatari.
West Ham walionekana kupooza katika mchezo
huo uliopigwa Jumatatu usiku, waliweza
kusawazisha bao kwenye dakika ya 77 kupitia kwa
Collins aliyeunganisha mpira uliokuwa una ambaa
kwenye lango la Chelsea.
Mabadiliko aliyoyafanya Conte kwa kuwaingiza
Victor Moses na Michy Batshuayi yaliongeza kasi
ya mashambulizi kwa upande wa Chelsea ambayo
ilifunga bao la ushindi kupitia Diego Costa dakika
moja kabla ya mpambano kumalizika.
Costa alipiga shuti kimo cha nyoka akiwa nje ya
18, mpira uliomshinda mlinda lango wa West Ham
Adrian na kutinga wavuni.
Huo ni ushindi muhimu kwa Conte, Meneja mpya
wa Chelsea kwani matokeo hayo yataimarisha
morali ya wachezaji wake.
Cesc Fabregas hakupata nafasi kwenye kikosi cha
kwanza cha Conte huku Pedro akiingia dakika 10
za mwisho za mchezo.
N'golo Kante aliyesajiliwa kutoka Leicester City
alianza kwenye mchezo huo na hakika amefanya
kile alichokuwa akikifanya wakati yuko Leicester.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni