0
Kuelekea Lala Salama ya Ligi Kuu
Soka Tanzania Bara Shirikisho La
Soka Nchini (TFF) limetoa onyo kali
kwa vilabu vinavyoshiriki Ligi hiyo
kutojihusisha na Aina yoyote Ya
upangaji wa matokeo na kuonya kuwa
hatua kali za kisheria zitachukuliwa
kwa watakaopatikana na hatia.
Akizungumza na mtandao huu Afisa
Habari wa TFF Alfred Lucas amesema
kuwa Wanaelewa upinzani uliopo kati
ya timu zinazowania kumaliza katika
nafasi ya Kwanza,tatu na nne na pas
pia zinazopambana zisishuke daraja.
Ushindani
-TFF tunaelewa hali ilivyo kwa sasa
tunajua kuna timu zinapambana
kumaliza katika nafasi ya kwanza kuna
kundi lingine ambalo wanapambana
kumaliza katika nafasi nne bora na Pia
kuna kundi la tatu ambao hao
wanapambana kubaki Ligi Kuu msimu
ujao, niwaonye kuwa TFF suala hili
tunalichukulia kwa uzito sana
Makamisaa na waamuzi ambao
watakuwa wanachezesha michezo
iliyobaki tunawaomba wawe makini na
wafanye kazi kwa kufuata sheria 17 za
soka" amesema Alfred Lucas.
Aidha ameongeza kuwa TFF itakuwa
na waangalizi (assessors) ili kuona
kuwa waamuzi hao na Makamisaa
wanazitafsiri vilivyo sheria hizo.
Waangalizi
-Tutakuwa na Assessors ambao
watakuwa katika kila uwanja wakati wa
Mechi ya Ili kuona sheria zote
zinatafsiriwa vilivyo la si hivyo hatua
kali zitachukuliwa kwa wale
wataonekana kujaribu kuharibu soka
letu" ameongeza Afisa Habari huyo.
Nafasi ya bingwa wa Ligi hiyo ikiwa
Bado wazi kwa Timu ya Simba na
Yanga Huku Nafasi ya tatu ikiwaniwa
na timu ya Azam, Kagera Sugar na
Mtibwa Sugar, wakati vita ya Kushuka
daraja inapiganwa na timu saba, za
Tanzania Prisons, Ndanda FC, Mbeya
City, African Lyon, Mbao FC, Toto
Africans, JKT Ruvu na Majimaji .
Ligi kuu Tanzania Bara Inatarajiwa
kufikia tamati Mei 11.

Chapisha Maoni

 
Top