0
Timu ya Azam Fc imewaonya Mbao
kutarajia kipigo cha aina yake
watakapokutana katika mchezo wa
Jumamosi.
 Afisa Habari wa Klabu ya Azam
Jaffary Iddi Mayanga, amesema
wamejianda vizuri na hawatatishika na
'Wagumu' hao kutoka Jijini Mwanza.
Timu nzuri
-Tuko vizuri tumefanya mazoezi ya
kutosha pointi tatu ni zetu tunaelewa
kuna upinzani lakini tumejipanga,
tunajua Mbao ni timu nzuri lakini
wanafanya vizuri wakiwa nyumbani
tuna matumaini ushindi ni wetu,
amesema Iddi.
Maganga amesema watakuwa makini
katika michezo iliobaki ili kulinda
heshima ya klabu hiyo.
Heshima
-Tutacheza kulinda heshima yetu
hata kama hatutashinda Ligi msimu
huu timu zitarajie upinzani mkali
kutoka kwetu, ameonya Maganga.
Michezo mitatu
Azam Fc ambao wako katika nafasi
ya tatu wakiwa na alama 46
wamebakiwa na michezo mitatu dhidi
ya Mbao Fc ,Toto Africans na Kagera
Sugar.

Chapisha Maoni

 
Top