0
Mbio za ubingwa wa Ligi kuu ya England kwa klabu ya Tottenham zimeingia doa baada ya kupoteza mchezo muhimu jana usiku dhidi ya West Ham United.
Tottenham ikicheza ugenini ilijikuta ikifungwa bao 1-0 bao la dakika ya 65 la kiungo wa West Ham Manuel Lanzini
Ni wiki moja tangu Tottenham ilipoifunga Arsenal nyumbani na kufufua matumaini ya kuweza kuizuia
Chelsea kuchukua ubingwa lakini kwa kufungwa jana Tottenham itawabidi sasa kuombea Chelsea nao wafungwe kwenye mechi yao ya Jumatatu hii
dhidi ya Middlesbrough.
Chelsea mpaka sasa inaongoza ikiwa na pointi 81 ikiwa imecheza mechi 34 wakati Tottenham wao wana piinti 77 baada ya mechi 35.

Chapisha Maoni

 
Top