0
Mshambuliaji Kinda wa Timu ya Azam
FC Shaban Idd Chilunda ambaye
alifunga mabao mawili katika ushindi
wa mabao 3-1 dhidi ya Mbao Fc
Katika mchezo wa Ligi kuu soka
Tanzania Bara, Amesema ushindi huo
umekuwa chachu katika vita ya
kugombani nafasi ya tatu.
Chilunda amesema anafurahi kuona
ameisaidia Timu yake kuibuka na
ushindi dhidi ya Timu ngumu ya Mbao
FC na kwamba kwa ushindi huo
watajitahidi kushinda ili kujiweka
katika nafasi nzuri ya kuikamata nafasi
ya Tatu.
-Tumepokea Vizuri matokeo haya, na
Ushindi huu umekuwa chachu kwa
michezo Miwili dhidi ya Toto Africans
na Kagera Sugar ambapo tukijipanga
vizuri tutaibuka na ushindi’ Alisema
Chilunda.
Mabao matano.
Chilunda ambaye Anavaa jezi nambari
43 na kujiunga Timu ya Wakubwa
msimu huu, ameifungia mabao
matano mpaka sasa huku akiwa na
umri wa Miaka 18.

Chapisha Maoni

 
Top