0
Klabu ya Singida United inatarajia
kuweka kambi ya Mwezi mmoja Jijini
Mwanza Kuanzia Mei 12, kwa ajili ya
kuchuja na Kusajili upya wachezaji
watakaotumika katika msimu ujao wa
Ligi kuu Soka Tanzania Bara.
Akithibitisha kuhusu Taarifa hiyo
Msemaji wa Klabu hiyo Elisante John
amesema sehemu kubwa ya Kambi
itahusisha wachezaji waliofanikisha
kuipandisha Singida United Ligi kuu
Pamoja na wachezaji ambao
wanatarajia kuwasajili baada ya Ligi
kuu Kumalizika.
-Ninafahamu kwamba Kambi itaanza
Mei 12 Jijini Mwanza, Kocha Hans
Van der Pluijm atakuja kuanza na
wachezaji walioipandisha Timu na
kuwachuja, ambapo tunatarajia zoezi
hilo lichukue hadi pale ligi kuu
itakapomalizika” Elisante Alisema.
Amesema kuna wachezaji wazuri
ambao sasa wanacheza ligi kuu
watajiunga na Kambi hiyo kwa ajili ya
kusajiliwa kama watamridhisha Kocha
lakini kwa sasa hawaoni sababu ya
Kuwaunganisha kwani wanaweza
kuleta migogoro na Vilabu vyao.
Nyota wa ligi kuu.
-Kuna wachezaji ambao kocha
alipendekeza tuwasajili, sasa
tunawaogopa kuwataja lakini
watajiunga na wenzao kwenye kambi
Jijini Mwanza, Na tunatarajia baada ya
Kambi ya Jijini Mwanza Basi kikosi
cha Singida United kinaweza kwenda
nchini Oman kwa ajili ya kuweka
kambi Maalumu ya Kuelekea Ligi kuu
soka Tanzania Bara’ Elisante
Aliongeza.
Singida United ni miongoni mwa Timu
tatu Ambazo zimepanda Daraja Msimu
huu kutoka Ligi daraja la Kwanza,
Timu nyingine ni Njombe Mji ya
Mkoani Njombe na Lipuli FC ya
Mkoani Iringa.

Chapisha Maoni

 
Top