0
Sasa iko wazi, mahakama ya
usuluhishaji wa masuala ya michezo,
CAS imepanga Agosti 25, mwaka huu
kuwa ndio siku ya kusikiliza rufaa
iliyowasilishwa na rais wa zamani wa
Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA),
Sepp Blatter ya kupinga kufungiwa
kujihusisha na masuala ya soka kwa
muda wa miaka 6.
Sepp Blatter mwenye miaka 80 na rais
wa zamani wa Shirikisho la Soka Ulaya
(UEFA), Michel Platini mwaka jana
walikutwa na hatia ya kuvunja maadili ya
kwa kuvuja paundi milioni 1 .3. Platini
alilazimika kujiuzulu mwezi wa 5 mwaka
huu ndani ya bodi hiyo ya soka Ulaya
baada ya kuungiwa miaka 6
kutokujishughulisha na masuala ya
michezo. Hata hivyo viongozi wote hao
wawili wanapingwa kushiriki kwenye
soka la aina yoyote.

Chapisha Maoni

 
Top