0
Jumla ya Wachezaji 45 wameteuliwa
kuunda Timu Mbili za Taifa za Soka
kwa Wanawake, ambapo Majina hayo
yametokana na Ligi ya wanawake
iliyomalizika Mwishoni mwa Mwezi
February Mwaka huu.
Akizungumza na Mtandao huu Kocha
wa Twiga Stars Edna Lema amesema
wachezaji hao wataingia wataitwa
katika Kambi ndogo ya Siku 7 ambapo
wakiwa hapo watachujwa kutokana na
Kiwango cha Soka na umri ili kuunda
Timu ya Taifa ya wakubwa na Timu ya
Vijana chini ya umri wa miaka 20.
Lema amesema wachezaji wengi
wanaounda Majina hayo 45 ni wapya
kabisa kutoka wale ambao walikuwa
wakiunda vikosi vya Twiga Stars na
U20 kwa miaka mingi.
-Wachezaji Hawa Tumewapata kutoka
katika ligi iliyomalizika, na Tulitaka
Tupate sura mpya, kwa hiyo asilimia
kubwa ni wachezaji wapya sio wale
ambao tulikuwa nao." Lema Alisema.
Kambi hiyo kwa Mujibu wa Kocha
Lema amesema itaanza mapema Mei
21 Jijini Dar es Salaam ambapo
itadumu Kwa Siku 7 na tayari
wametuma maombi kwa walezi,
Walimu na Wazazi wa wachezaji hao
ili waweze kuwaruhusu kujiunga na
Kambi hiyo.
Kambi nyingine.
Amesema kwa wachezaji ambao
watakuwa bado hawajamaliza mitihani
kwa Maana ya wale wale mashuleni,
wataangalia namna ya kuwatafutia
Siku nyingine ili waweze kufanya
program Sawa na wenzao na
kuteuliwa katika Timu hizo mbili.
-Tumeandika Barua kwa
waliomashuleni ili wapate ruhusa, Ila
kuna wengine ambao watakuwa
hawajamaliza mitihani, tutashindwa
kuwatumia kwa sababu hatuwezi
kuwaharibia mitihani, hivyo kama
kutakuwa na Camp nyingine basi wale
ambao hawakupata nafasi tutawaita
kwa ajili ya Kuwaangalia" Lema
aliweka wazi.
Katika hatua nyingine Lema amesema
kwa wale ambao watashindwa
kuchaguliwa wasiogope Kwani
kumbukumbu zao zitatunzwa na
ikitokea wanahitaji huduma ya
mchezaji basi hawatahangaika sana
zaidi ya kuwafuata hao.

Chapisha Maoni

 
Top