0
Kampuni ya Bahati Nasibu ya
SportPesa imeingia mkataba wa miaka
Mitano na Klabu ya Dar Young
Africans ambapo utawafanya Yanga
kulipwa Milioni 950 kwa Mwaka.
Akizungumza wakati wa Utiliwaji Saini
Mkurugenzi wa Utawala wa kampuni
ya SportPesa Abass Tarimba
amesema Yanga watapata Fedha hizo
nahamishia Ongezeko la Asilimia 5
kila mwaka.
-Yanga watapata shilingi Milioni 950
kwa miaka 5 na ongezeko la asilimia
5 kila mwaka kuifanya thamani ya
mkataba kuwa bilioni 5" Alisema
Tarimba.
Tarimba Ameongeza kuwa udhamini
huo utaifanya Yanga kuendelea kuwa
na Nguvu ya Kisoka katika Ukanda wa
Afrika Mashariki na Kati.
Bonasi ya Milioni 100.
-Udhamini huu utaifanya Yanga
iendelee kuwa na Nguvu Zaidi na
Zaidi na Kama Yanga Atakuwa bingwa
wa Tanzania atapata bonasi ya shilingi
mil 100" Aliongeza Tarimba.
Aidha Yanga baada ya kupata
udhamini huo wameshindwa kujibu
hoja ya wapi wataiweka nembo ya
Mdhamini wao wa sasa ambao ni
Quality Group na kusema kwamba
watatolea ufafanuzi siku nyingine.

Chapisha Maoni

 
Top