0
Tetesi za kumhusisha Griezmann na klabu nyingine zimefungwa rasmi msimu huu baada ya Mfaransa huyo kumwaga wino kubaki Atletico hadi 2022
Antoine Griezmann ameongeza mkataba kuendelea kuitumikia Atletico Madrid hadi majira ya joto 2022.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alihusishwa na tetesi za kutua Manchester United mwishoni mwa mwezi uliopita, Mashetani Wekundu nao wakijiamini kuwa wangempata kwa paundi milioni 87.
Mazungumzo hayo kuhusu kutua kwake Old Trafford yaliingia shakani, hata hivyo, ilipothibitika kwamba rufaa ya Atletico dhidi ya adhabu ya kufungiwa imeshindikana, ilikuwa wazi kwamba hawawezi kusajili mchezaji mwingine na kwa maana hiyo hawawezi kuuza wachezaji wao muhimu majira ya joto.
Griezmann alituma ujumbe wa twitter
'sasa ni zaidi ya mwanzo ' kuthibitisha kwamba anabaki Atletico mapema mwezi huu, na mshambuliaji huyo ameshasaini mkataba mpya na miamba wa Madrid.
"Jambo la kwanza, nataka kuomba radhi kwa taarifa zinazokangannya," Griezmann aliiambia tovuti rasmi ya Atletico.
"Labda nilijieleza vibaya au mtu fulani alitaka kutengeneza habari ilihali hapakuwa na habari, lakini tangu nilipotua hapa, nilijitoa kwa ajili ya klabu, kwa wachezaji wenzangu na benchi langu la ufundi, na nafurahia kuishi msimu mwingine zaidi pamoja nayi nyote."
Kiasi cha paundi milioni 87 kinachohitajika kuvunja mkataba wa Griezmann kitabaki kama kilivyo, ingawa inafahamika kuwa makubaliano mapya ya mkataba yamemfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika historia ya klabu.

Chapisha Maoni

 
Top