Klabu ya Kagera Sugar ya Mjini Bukoba Mkoani Kagera imetangaza rasmi kuwasajili wachezaji Sita akiwemo mchezaji wa zamani wa Timu ya Simba na Mbeya City Juma Said Nyosso.
Usajili huo umetangazwa na Kiongozi wa Timu hiyo Mohammed Hussein na kusema kuwa wachezaji wote waliosajiliwa ni pendekezo la Kocha Mecky Mexime kwa ajili ya Msimu ujao.
Nyosso anasajiliwa Kagera Sugar baada ya kumaliza adhabu yake ya kufungiwa miaka miwili kufuatia kumtomasa makalio mshambuliaji John Raphael Bocco akiwa Azam FC kabla ya kuhamia Simba wiki hii.
wengine waliosajiliwa.
Mbali na Nyosso ambaye alifungiwa akiwa anachezea Mbeya City mwaka juzi, Mohammed Hussein Amesema Klabu yake pia imemsajili kipa Hussein Kipao kutoka JKT Ruvu iliyoshuka Daraja pamoja na Japhary Kibaya kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro
aidha Kagera Sugar pia imemtangaza Kiungo Peter Samson Mwalyanzi na Ludovic Venance na mshambuliaji Omary Daga maarufu ‘Dagashenko’ wote kutoka Africa Lyon iliyoshuka Daraja pia.
Mbali na kuwasajili wachezaji hao lakini pia Mohammed Hussein amesema kuwa wamemuongezea mkataba wa mwaka mmoja mlinda mlango Juma Kaseja baada ya kuwa na msimu mzuri katika ligi iliyomalizika hivi karibuni.
Mohammed Hussein amesema wamefanya usajili huo pamoja na kuwabakiza waliofanya vizuri msimu uliopita wakiwa na lengo la kushika nafasi mbili za juu katika msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania Bara.
-Nia yetu ni kusika nafasi mbili za juu katika msimu ujao wa ligi na ndio maana tumeanza usajili huu mapema na tunaamini kuwa kile ambacho tumedhamiria kitafanikiwa, tulitaka kuwabakisha wachezaji wetu waliofanya vizuri na hilo tumefanikiwa kwa asilimia zaidi ya 90" Alisema Hussein
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.