0
UONGOZI wa Singida United uliahidi kununua magari madogo kwa ajili ya wachezaji wao na sasa mambo yameiva kwani magari hayo yamewasili bandarini Dar es Salaam yakisubiri taratibu za kutolewa.
Ingawa Singida United imenunua basi kubwa kwa ajili ya timu, lakini magari hayo watapewa wachezaji ambapo watakuwa wakiyatumia kwenye shughuli zao binafsi wanapokuwa kwenye mapumziko.
Katibu Mkuu wa Singida United, Abdulrahiman Sima, ameliambia Mwanaspoti: “Tunasajili wachezaji saba wa kigeni, huo ndiyo mpango wetu na haujabadilika, hao wageni tutawapa magari ambayo tayari yameingia bado kuyatoa, ila si kwamba kila mtu atapewa gari lake bali kila gari litakuwa linatumika na wachezaji wawili ama watatu.
“Hata hawa wachezaji wazawa watapata magari ambayo pia watakuwa wakiyatumia kwa kushirikiana, tunawapa magari hayo ili kuwarahisishia kwenda kufanya shughuli zao binafsi wanapokuwa kwenye mapumziko kwani hawawezi kutumia magari ya timu kwani ni makubwa, hivyo tunafanya taratibu za kuyatoa.”

Chapisha Maoni

 
Top