0
Timu ya Soka ya Simba inatarajiwa kutangaza hivi karibuni kumsajili Mshambualiaji hatari kutoka Zambia Walter Bwalya ambaye kwa sasa anakipiga na timu ya Nkana inayoshiriki ligi Kuu Soka nchini humo.
Bwalya alimaliza Msimu uliopita wa FAZ super Division akiwa na mabao 24 na anakuja nchini akiambatana na Mshambuliaji wa Uganda Emmanuel Okwi kwa lengo la kuimarisha safu ya ushambuliaji ya timu hiyo msimu ujao.
Taarifa ndani ya klabu hiyo zinasema kwamba Aliyefanikisha dili hilo ni Mfanyabiashara Mohamed Dewji 'MO' ambaye ni kipenzi cha mchezaji huyo kwa muda mrefu pamoja na kuendeleza nia yake ya kuisaidia Simba.
Bwalya ambaye uraia wake Bado unawachanganya wengi Kwani amezaliwa na Mama Mkongo na Baba Mzambia anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili.
Ikumbukwe kwamba Kocha George Lwandamina aliwahi kumuita Bwalya kwenye kikosi cha Timu ya Taifa Kabla ya kuenguliwa kutokana na matatizo ya Uraia wake.
Safu ya ushambuliaji.
Kama Bwalya pamoja na Okwi watatua Simba, Basi kikosi hicho cha wekundu Wa Msimbazi kitakuwa na safu kali zaidi ya ushambuliaji ikiongoza na Laudit Mavugo, John Bocco, Juma Luizio na Ibrahim Ajib.

Chapisha Maoni

 
Top