0
Timu ya Yanga imeanza usajili wake kwa kumsajili mchezaji Abdallah Shaibu ‘Ninja’ aliyekuwa anakipiga katika timu ya Taifa Jang’ombe inayoshiriki katika Ligi Kuu ya nchini Zanzibar kwa mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia klabu hiyo.
Usajili huu unamaanisha kuwa klabu ya Yanga imeanza safari yake usajili baada ya kukaa kimya huku vilabu vya Simba na Azam wakionyeshana ubabe baada ya kuwasajili nyota kadhaa waliotamba katika Ligi Kuu.
Beki huyo inasemekana kuwa ameenda Yanga kuziba pengo la Nadir Haroub ‘Canavaro’ ambaye soka lake lipo ukingoni katika kikosi hicho.

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top