Everton imeanza harakati za kuisaka saini ya mshambuliaji wa Crystal Palace, Christian Benteke, kwa mujibu wa chanzo cha Sky.
Klabu hiyo ya Merseysiders tayari imewasajili washambuliaji wawili Sandro Ramirez na Wayne Rooney msimu huu, lakini sasa wanaonekana wanamtaka mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool, Benteke.
Taarifa zinadai kuwa mshambuliaji huyo ambaye ameighalimu Palace rekodi ya uhamisho wa pauni 27milioni, anaweza kuondoka.
Kocha wa Ronald Koeman alikuwa akitafuta mshambuliaji wa kuziba pengo la Romelu Lukaku, ambaye amekamilisha uhamisho wake wa kwenda Manchester United kwa gharama ya pauni 90milioni.
Benteke, ambaye naye natajwa kutakiwa na Chelsea, aliondoka Liverpool na kuhamia Selhurst Park msimu uliopita ambako alifunga mabao 17 akiwa chini ya kocha Sam Allardyce.
Chapisha Maoni