Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dokta Harrison Mwakyembe, amesitisha uteuzi wa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa ‘BMT’ Dioniz Malinzi pamoja na wajumbe wote wa Baraza hilo.
Katika Taarifa kwa Vyombo habari leo Julai 10, Mwakyembe amesema kwamba Sekretarieti ya Baraza hilo itaendelea kufanya kazi kwa kushirikiana kwa karibu na wizara wakati taratibu za kumpata mwenyekiti na wajumbe Wapya zikiendelea kufanyika kwa Mujibu wa Sheria.
Waziri Mwakyembe ametumia Sheria ya BMT namba 12 ya Mwaka 1967( Kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria namba 6 ya 1971) Pamoja na kanuni zak za 1999 kusitisha uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wote wa Baraza.
Katika Taarifa Hiyo Mwakyembe amesema BMT imegubikwa na migogoro ya mara kwa mara ambayo imechangia sana kudumaza maendeleo ya Michezo nchini.
Matumaini ya Serikali.
Anasema Serikali ya Awamu ya Tano ilitarajia kwamba kupitia BMT, Migogoro hiyo ingeweza kupatiwa ufumbuzi wa kudumu kwani Baraza hilo limepewa jukumu la kushughulikia masuala yote yanayohusu michezo ikiwa ni pamoja na weledi, amani, utulivu na utawala bora katika Tasnia ya Michezo.
Mwakyembe ameeleza kuwa mbali na jitihada ambazo BMT imekuwa ikizifanya Toka lilipoteuliwa mwaka 2015 lakini kunahitajika mikakati mipya na nguvu mpya ili kuona tasnia hiyo ya Michezo nchini kama yalivyomatarajio ya wengi ikileta tija.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Hatua Hiyo imekuja Siku chache toka Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majali alipomuagiza waziri Mwakyembe kulifanyia mapitio na kulitathimini Upya BMT ili kujiridhisha na usimamizi wake wa shughuli za Michezo Nchini kama itakuwa vinginevyo anaweza kulivunja lililopo na Kuunda Jipya.
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ni Shirika la Umma lililoundwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Sheria Na.12 ya Mwaka 1967 na Marekebisho yake Na. 6 ya 1971 ya Baraza la Michezo la Taifa. Baraza la Michezo la Taifa limepewa jukumu la kusimamia michezo yote Tanzania, ukiwemo Mpira wa Miguu.
Chapisha Maoni