0
Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga amemuita kikosini aliyekuwa kipa wa timu ya taifa ya vijana 'Serengeti Boys', Ramadhan Kabwili katika maandalizi ya mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) dhidi ya Rwanda, Jumamosi hii.
Kabwili ameitwa kikosini kuchukua nafasi ya Beno Kakolanya aliyeumia.
Mbali na Kabwili, wachezaji wengine walioongezwa ni Said Ndemla, Joseph Mahundi, Athanas Mdamu na Boniface Maganga.
Kocha Salum Mayanga pia ameongeza katika kikosi hicho Said Ndemla, Joseph Mahundi, John Bocco na Kelvin Sabato.
Mayanga alisema amewaongeza hao baada ya kuwaondoa kikosini washambuliaji Elius Maguli na Thomas Ulimwengu kutokana na kucheza nje ya nchi pia kutokana na majeruhi ya wachezaji wengine.
Tanzania itacheza mechi ya kwanza ya kusaka kufuzu kwa CHAN 2018, Kenya dhidi ya Rwanda jijini Mwanza na kurudiana Kigali Rwanda.
Mshindi wa mechi hiyo atacheza dhidi ya mshindi wa mchezo kati ya Uganda inayopewa nafasi kubwa ya kuifunga Somalia au Sudan Kusini watakayocheza nayo.

Chapisha Maoni

 
Top