Wakati Kocha Arsene Wenger akiwa kwenye vita ya kuimarisha kikosi chake, ameigeukia klabu ya Manchester City na kuionya kuhusu chokochoko walizozianzisha za kutaka kumsajili mshambuliaji wake, Alexis Sanchez.
Wenger amekuwa kwenye mikakati ya muda mrefu ya kutaka kumsajili Kylian Mbappe ili kukiongezea makali kikosi chake lakini klabu yake imetamka kwamba mchezaji huyo hatoki msimu huu.
Pia, amefanikiwa kumbakisha Sanchez kikosini hapo kwa mkataba wa mwaka mmoja jambo ambalo Manchester City wametumia mwanya huo kuanza kumshawishi.
Hata hivyo, mkwara huo wa Wenger unaonekana ni kama nguvu ya soda kwa sababu kipindi kilichopita, alionya kuhusu klabu yoyote inayomuwinda Robin van Persie hata hivyo mwishowe akahamia Manchester United.
Chapisha Maoni