Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wao wa kufuzu kwa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan)dhidi ya Rwanda.
Stars ilitua jijini hapa jana Jumatatu saa 2:30 usiku na ndege na Fastjet kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo unaotarajia kufanyika Julai 15 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Mayanga alisema kikosi alichonacho anaamini kinaweza kufanya vizuri kama ilivyokuwa katika mashindano ya Cosafa.
Aliongeza kuwa Rwanda ni timu bora katika ukanda wa Afrika Mashariki, hivyo watajituma zaidi na kupambana kwa hali yoyote kuhakikisha wanasonga mbele.
“Tumejipanga vizuri na tunaamini tutashinda mchezo huo licha ya kwamba Rwanda ni timu bora kwahiyo tutajituma kwa namna yoyote kuhakikisha tunashinda,” alisema Mayanga.
Viingilio katika mchezo huo ni 5,000 (mzunguko),10,000 (bandani) na wanafunzi Sh 1,000, ambapo wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu ya Taifa,Jumamosi.
Chapisha Maoni