Mashabiki wa soka wa Tanzania watapata nafasi ya kumtazama mshambuliaji mpya wa Everton, Wayne Rooney akiongoza timu hiyo dhidi ya Gor Mahia kwa kiingilio cha Sh 3000 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Everton itawasili nchini kesho asubuhi wakata mabingwa wa Kombe la SportPesa, Gor Mahia ya Kenya imewasili leo mchana tayari kwa mchezo huo Alhamisi.
Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema kiingilio cha chini kitakuwa sh 3000 wakati VIP C itakuwa sh 8000 na VIP A na B kutakuwa na utaratibu maalumu.
Meneja miradi wa kampuni ya Selcom, Gallus Runyeta alisema tiketi zitaanza kuuzwa leo, Jumanne kwa njia ya mtandao, pia mawakala wao watakuwepo Alhamisi siku ya mchezo wakiuza tiketi nje ya uwanja.
Pia, Lucas aliwataja waamuzi watakaochezesha mchezo huo kuwa ni Israel Nkongo atasaidiana na Ferdnand Chacha na Frank Komba wakati mwamuzi wa akiba atakuwa ni Elly Sasii huku kamishna wa mchezo akiwa ni Michael Wambura.
Chapisha Maoni