0

Hatimaye Alexandre Lacazette ametua Arsenal baada ya kukamilisha mipango ya uhamisho wake wenye thamani ya Pauni 52 milioni kutoka Lyon.
Lacazette, 26 aliwasili kwenye uwanja wa mazoezi wa Arsenal jana mchana tayari kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.
Nyota huyo aliyeifungia klabu yake, Lyon mabao 37 msimu uliopita atalipwa mshahara wa Pauni 150,000 kwa wiki.
Huo, utakuwa usajili kwa kwanza mkubwa wa kocha Arsene Wenger ambaye ana kibarua cha kuwabakisha kundini waasi Hector Bellerin na Alexis Sanchez wanaotaka kuondoka.
Mshambuliaji huyo Mfaransa anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano kuichezea Arsenal na pengine atamwondoa Olivier Giroud anayetakiwa na klabu kadhaa za England, West Ham na Everton.
Rais wa Lyon, Jean- Michel Aulas alisema juzi kuwa uhamisho wa Lacazette ambaye alitambulishwa kwa wenzake waliowasili kuanza maandalizi ya msimu mpya, utakamilika ndani ya saa 48.
Aulas alitamba kuwa ni faraja kuona mchezaji wao amenunuliwa kwa zaidi ya Euro 45 milioni.


Chapisha Maoni

 
Top