0
Cristiano Ronaldo ameanza mazoezi kwa mara ya kwanza na timu yake mpya ya Juventus tangu alipokamilisha uhamisho wake wa pauni 99milioni kutoka Real Madrid .
Mreno huyo mwenye miaka 33, alionekana akiwa mazoezini na wachezaji wenzake katika maandalizi yao ya msimu mpya..
Ronaldo sasa amepata nafasi ya kuonekana uwanjani akiwa na jezi ya timu yake mpya katika maandalizi ya Serie A.
Mshambuliaji huyo ametwaa mataji manne ya Ligi ya Mabingwa na mawili ya La Liga akiwa na kikosi cha Real Madrid.
Sasa anajiandaa kuanza maisha mapya akiwa na timu mpya kwa mara ya kwanza tangu 2009 baada ya kuondoka Madrid na kutua Turin.
Ronaldo alifanya mazoezi ya viungo na kukimbia katika mazoezi ya asubuhi leo na kuonyesha ishara ya vidole viwili kwa wapiga picha waliokuwepo uwanjani hapo.

Chapisha Maoni

 
Top