0
BAO pekee la Gerard Pique limeipa Barcelona ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Cypriots Apoel Nicosia ya Cyprus usiku huu katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Pique alifunga bao muhimu akimalizia mpira wa adhabu wa Lionel Messi katikati ya kipindi cha kwanza, lakini Apoel iliwabana vilivyo
Barca licha ya kuongozwa na nyota wake Messi na Neymar mbele.

Katika mchezo mwingine, Luka Zahovic
alitokea benchi kuinusuru Maribor kulala
Sporting kwa kupata safe ya 1-1 kwa bao la dakika ya mwisho baada ya Luis Nani kutangulia kuwafungia wapinzani wao.

Chapisha Maoni

 
Top