







Maafisa usalama nchini Ufaransa wamemaliza operesheni za tukio la utekaji nyara wa watu, katika duka la dhahabu na taasisi ya uchapishaji
vitabu huko mashariki na kaskazini mwa mji mkuu, Paris kwa kuwaua wahusika wa utekaji nyara huo.
Jana polisi walifanya msako kuwasaka ndugu wawili wanaotuhumiwa kuhusika katika shambulizi kwenye ofisi ya gazeti la Charlie Hebdo ambalo mwaka 2011 lilichapisha mara kadhaa vibonzo na
vikatuni vinavyomvunjia heshima Mtume Mtukufu Muhammad SAW. Katika tukio hilo polisi waliwakomboa pia mateka bila ya kupata madhara.
Katika tukio jingine maafisa usalama wa Ufaransa walifanya operesheni nyingine ya kuwakomboa mateka waliokuwa wamezuiliwa katika duka moja
mjini Paris operesheni ambayo imepelekea kwa uchache watu watano kuuawa.
Operesheni hizo zilifanyika jana Ijumaa kwa minajili ya kuwatia mbaroni ndugu hao wawili, Said na Sharif Kawashi, raia wa Ufaransa wanaotuhumiwa kuhusika katika shambulizi la siku ya Jumatano katika gazeti la Charlie Hebdo,
ambapo watu 12 waliuawa.
Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Ufaransa, Manuel Valls amekiri udhaifu wa idara ya upelelezi ya nchi
yake katika matukio hayo yaliyopelekea kuuawa raia 14 na askari watatu katika matukio ya siku tatu zilizopita.
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.