0
Jumla ya shilingi bilioni 1.3 zimekusanywa kutoka Daraja la Nyerere lililopo Kigamboni jijini Dar es
Salaam kupitia tozo mbalimbali zinazolipwa na vyombo vya usafiri vinavyopita darajani hapo.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Prof. Godius Kahyarara wakati akieleza mapato yaliyopatikana
kwenye daraja hilo tangu lilipofunguliwa rasmi Mei 14 mwaka huu.
Prof. Kahyarara alisema kuwa fedha hizo
zimekusanywa kupitia tozo za magari yakiwemo magari binafsi, magari ya abiria, magari ya mizigo,
pikipiki na bajaji zinazopita darajani hapo kila siku.
Kwa upande wake Msimamizi wa Mradi wa Darajl la Nyerere, Bw. Gerald Sondo alisema kuwa
Serikali kwa kushirikiana na uongozi wa daraja
wana mpango wa kuboresha huduma za malipo ili watumiaji wa daraja hilo waweze kulipa tozo kwa
kutumia kadi za kielektroniki.
“Hivi karibuni tunatarajia kuanzisha mfumo wa
malipo kwa kutumia kadi za kielektroniki ambapo
madereva wa vyombo vya usafiri watakuwa
wanatumia kulipa tozo pindi wanapopita darajani”
alisema Sondo.
Aliongeza kuwa mfumo huo utapunguza
changamoto ya kupokea pesa taslimu mkononi
kwa wanaokusanya mapato darajani hapo, hivyo
kuondoa usumbufu wa chenji na kuimarisha
usalama wa fedha hizo.
Aidha, Bw. Sondo alieleza kuwa mfumo huo pia
utawawezesha watumiaji wa daraja hilo kulipa tozo
kwa kutumia mifumo ya kielektroniki ya kufanya
miamala ya fedha kupitia benki na mitandao
mbalimbali ya simu.
Alisema kuwa kwa sasa idadi ya magari, pikipiki
na bajaji zinazopita darajani hapo ni kati ya elfu 8
hadi elfu 10 kwa siku na wanalipa tozo kulingana
na aina ya chombo cha usafiri.
Kwa upande wa waenda kwa miguu na waendesha
baiskeli hawalipi gharama yoyote wanapopita
kwenye daraja hilo.
Akieleza kuhusu usalama wa daraja na watumiaji
wake, Bw. Sondo alisema kuwa ulinzi ni wa
uhakika kwa saa 24 kila siku kwani kuna askari wa
kutosha pamoja na kamera zinazosaidia zoezi hilo.
Pia alisema kuwa wanaandaa kanuni za matumizi
ya daraja ikiwemo faini za uharibifu, uchafuzi wa
mazingira, matumizi mabaya ya njia na lugha za
matusi.




EATV

Chapisha Maoni

 
Top