0
MSHAMBULIAJI Gervinho na Nahodha
mkongwe wa umri wa miaka 37, Francesco Totti wamefanya kazi nzuri usiku huu AS Roma ikiifumua CSKA Moscow mabao 5-1 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa
Olimpico.

Gervinho amefunga mabao mawili na kuseti lingine moja lililofungwa na mchezaji mpya, Juan Iturbe wakati mabao mengine yamefungwa na Maicon na Totti, wakati bao pekee la CSKA limefungwa na Ahmed Musa.
Bahati mbaya kwao Roma, Iturbe aliumia
kipindi cha kwanza na kutoka.

Katika michezo mingine, Athletic Bilbao
imelazimishwa safe ya 0-0 na Shakhtar
Donetsk wakati Porto iliichapa 6-0 BATE jana.

Chapisha Maoni

 
Top